AFGHANISTAN-QATAR

Rais wa Afghanistan kufanya ziara nchini Qatar kwa mazungumzo na wawakilishi wa Taliban

Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai
Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai REUTERS/Syrian TV via Reuters TV

Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai wiki hii anatarajiwa kuzuru nchi ya Qatar kwa mazungumzo ya kuangalia uwezekano wa kufunguliwa kwa ofisi mpya za wanamgambo wa Talibana kama njia ya kutafuta suluhu nchini humo. 

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya mambo ya nje wa Afghanistan imesema kuwa rais Karzai atakuwa nchini Qatar kwa mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo na wale wawakilishi wa kundi la Taliban kuangalia uwezekano huo wa kufungua ofisi.

Taarifa hiyo inatolewa wakati ambapo imepita miezi kadhaa toka rais Hamid Karzai mwenyewe apinge wazo wa kundi la Taliban kuwa na ofisi nchini Qatar kwa madai kuwa hakutakuwa na mantiki yoyote.

Kubadilika msimamo kwa serikali ya rais Karzai huenda kukawa kumechangiwa na shinikizo toka kwa nchi ya Marekani ambayo mara zote imetaka kuwepo mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Serikali ya Afghanistan na wapiganaji wa Taliban.

Hata hivyo kundi la wanamgambo wa taliban limekataa kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na rais Karzai kwa kile lilichoeleza kuwa amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna muafaka nchini humo.

Kauli ya Taliban napingwa vikali na wizara ya mambo ya nje ambayo inasema itafanya mazungumzo na Taliban iwapo itaacha uhusiano wowote ilionao na kundi la mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda.