PAKISTAN

Rais wa zamani wa Pakistan, Pervez Musharraf arejea nchini mwake baada ya kuishi uhamishoni kwa zaidi ya miaka 4

Rais wa Zamani wa Pakistan, Pervez Musharraf amerejea nchini mwake siku ya Jumapili baada ya kuwa anaishi uhamishoni nchini Uingereza kwa zaidi ya miaka minne toka alipoondoka madarakani. 

Rais wa zamani wa Pakistan, Pervez Mushar
Rais wa zamani wa Pakistan, Pervez Mushar Reuters
Matangazo ya kibiashara

Musharraf anarejea nchini humo licha ya kitisho toka kwa wapiganaji wa kundi la Taliban ambao walitishia kumuua iwapo angerejea nchini humo kwa kile kundi hilo ilichoeleza kuwa ni msaliti wa taifa lake.

Punde mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Karachi na kuwahutubiwa maelfu ya wafuasi wake, Musharraf amesema kuwa ameamua kurejea nchini mwake kuthibitisha kuwa haofii uhai wake na kwamba amekuja kuikomboa nchi hiyo.

Musharraf anarejea nchini humo wakati huu ambapo nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wae mkuu wa kwanza wa kidemokrasia tarehe 11 ya mwezi may, uchaguzi ambao Musharraf anatarajiwa kusimama kuwania nafasi ya urais.

Licha ya kukabiliwa na tuhuma za rushwa dhidi yake na matumizi mabaya ya ofisi, Musharraf ameendelea kusisitiza kutokuwa na hatia kuhusu tuhuma ambazo zinamkabili na ndio maana ameamua kurejea nchini mwake.

Bunge la nchi hiyo limemteua jaji mstaafu, Mir Hazar Khan Khoso kuwa waziri mkuu wa muda kuelekea uchaguzi mkuu.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa licha ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili kiongozi huyo, bado anapewa nafasi kubwa ya kuweza kuibuka na ushindi kwenye uchaguzi wa mwezi May.