ZAMBIA

Rupiah Banda aiambia mahakama hana hatia, kesi yake kuanza kusikilizwa April 3

Aliyewahi kuwa rais wa Zambia, Rupiah Banda ambaye siku ya Jumanne alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, amekana mashtaka yanayomkabili na kusisitiza kuwa hana hatia.

L'ex-président Rupiah Banda (c) quitte le palais de justice après avoir plaidé non coupable. Lusaka, le 26 mars 2013.
L'ex-président Rupiah Banda (c) quitte le palais de justice après avoir plaidé non coupable. Lusaka, le 26 mars 2013. Photo AFP / Joseph Mwenda
Matangazo ya kibiashara

Akisimama mbele ya hakimu Joshua Banda, kiongozi huyo baada ya kusomewa mashtaka yake na kuulizwa iwapo anyakubali, alisimama na kusema kuwa hana hatia ya makosa ambayo ameshtakiwa nayo.

Kesi dhidi ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi inayomkabili Rupiah Banda, imepangwa kuanza kusikilizwa rasmi tarehe 3 ya mwezi April ambapo upande wa mashtaka unatarajiwa kuwasilisha ushahidi wake kudhibitisha makosa dhidi ya Banda.

Rupiah Banda alikamatwa siku ya Jumatatu na kupandishwa kizimbani kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ambapo mara zote Banda amesisitiza kuwa hana hatia dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Banda anatuhumiwa kwa kushiriki vitendo vya rushwa akiwa kama rais kwa kutia saini mkataba wa mafuta na kampuni moja nchini Nigeria pamoja na kutumia madaraka yae vibaya akiwa kama rais.

Mawakili wanamtetea Banda wameendelea kusisitiza kuwa mashtaka dhidi ya mteja wao yanashinikizo la kisiasa na kwamba watahakikisha wanathibitisha mteja wao hana hatia juu ya makosa yanayomkabili.