CYPRUS-EU-ECB-IMF

Wananchi wa Cyprus waendelea na maandamano kupinga mpango wa nchi yao kupatiwa mkopo

Maelfu ya wananchi wa Cyprus wakiandamana kupinga mpango wa nchi yao kupatiwa mkono na Umoja wa Ulaya
Maelfu ya wananchi wa Cyprus wakiandamana kupinga mpango wa nchi yao kupatiwa mkono na Umoja wa Ulaya Reuters/Yorgos Karahalis

Maandamano yameendelea nchini Cyprus huku wananchi wengi wakipinga mkopo ulioidhinishwa na Umoja wa Ulaya EU kusaidia kuokoa uchumi wa Taifa hilo ambao umetetereke. 

Matangazo ya kibiashara

Maandamano kwenye mitaa mbalimbali nchini Cyprus yameanza kuwa kitu cha kawaida kipindi hiki ambacho wananchi wenye hasira wakipinga hatua ya Taifa lao kupewa mkopo wa Umoja wa Ulaya EU ili ijinasue na hali ngumu.

Kumekuwa na hali tete kwenye maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kutokana na wananchi kuwa vinara wa kupinga kwa nguvu zao zote hatua ya Umoja wa Ulaya EU na Shirika la Fedha Duniani IMF kuipa masharti nchi hiyo ili iipatie mkopo.

Serikali imeridhia hatua hiyo ya kupatiwa mkopo kutoka kwa Umoja wa Ulaya EU na IMF lakini Bunge la Taifa hilo likigawanyika juu ya kuridhia au kupinga masharti yaliyotolewa na Taasisi hizo zilizotayari kunusuru uchumi wa Taifa hilo.

Wananchi wameingia mitaani kupinga hatua hiyo huku mabenki yakitarajiwa kufunguliwa hiyo kesho baada ya kufungwa kwa kipindi cha siku kumi lengo likiwa ni kuhakikisha wanadhibiti uchukuaji wa fedha.

Mabenki nchini Cyprus yalilazimika kufungwa baada ya wananchi wengi kujitokeza na kutaka kutoa fedha zao baada ya kusikia kuna mchakato wa kuanza kutoza ushuru kwa wale wote watakaokuwa wanatoa fedha zao.

Hatua hiyo ya utoaji wa fedha kwa kiasi kikubwa ndiyo unatajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa uchumi pamoja ya kupungua kwa mzunguko wa fedha ambao umechangia hali ngumu ya maisha.

Maandamano hayo yamechangia kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Cyprus Andreas Artemis akiwa ni miongoni mwa wale wanaopinga mchakato wa marekebisho ya kibenki yaliyopendekezwa na Umoja wa Ulaya EU.

Benki wa Cyprus ndiyo inatarajiwa kufunguliwa kesho huku Benki maarufu ya Laiki yenye weteja wengi ikitarajiwa kufilisiwa kama moja ya hatua ya kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa kibenki na wananchi wengi wakitarajiwa kupoteza ajira.

Wananchi wanapinga hatua ya kufungwa kwa Mabenki mengine wakiamini hatua hiyo itasababisha wananchi wengi kupoteza ajira zao za kudumu kitu ambacho kinaweza kikaleta mtikisiko wa uchumi na shughuli za uzalishaji.