KOREA KASKAZINI-MAREKANI-KOREA KUSINI

Marekani yatuma ndege aina ya B-2 kwenye pwani ya Korea Kusini tayari kukabiliana na kitisho cha Korea Kaskazini

Nchi ya Marekani imetuma ndege maalumu aina ya B-2 zenye uwezo wa kuzuia mashambulizi ya Nyuklia nchini Korea Kusini ikiwa ni hatua nyingine inayoelezwa itachochea mzozo zaidi kati yake na Korea Kaskazini. 

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akitazama zana mpya ya kijeshi
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akitazama zana mpya ya kijeshi REUTERS/KCNA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya nchi hiyo, imethibitisha ndege zake kusafiri umbali wa maili elfu kumi na tatu kwenye pwani ya Korea Kusini ikiwa ni mazoezi yanayoendelea kati ya Marekani na Korea Kusini.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa jaribio la ndege hizo kunaonesha uwesho wa Marekani na washirika wake kuwa tayari kukabiliana na hatari yoyote ambayo inaweza kufanywa na Korea Kaskazini ambayo imetishia kushambulia kambi zake za kijeshi za Hawaii.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa hatua ya Marekani kutuma ndege hizo kutaendelea kuchochea moto ambao umeanza kuwaka kati ya nchi za Korea Kusini na Kaskazini ambazo zimeingia kwenye mzozo wa kijeshi hivi sasa.

Hapo jana Serikali ya Pyongyang ilitangaza kukata mawasiliano yote ya kijeshi na majirani zake wa Korea Kusini kwa kile ilichoeleza kuwa ni kuchoshwa na vitisho vya majirani zake na Marekani kuhusu mpango wake wa Nyuklia.

Kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-Un amekuwa akitembelea kambi za jeshi la Korea Kaskazini katika mpango unaoelezwa ni kujiweka tayari kwa nchi hoyo kwa vita na nchi za Marekani na Korea Kusini.

Nchi hiyo imetishia kutumia silaha za nyuklia kushambulia kambi za kijeshi za Hawaii na Guam nchini Marekani iwapo mazoezi ya kijeshi kati yao na Korea Kusini hayatasitishwa.