MANDELA-AFRIKA KUSINI

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela akimbizwa hospitalini kwa matibabu

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, mzee Nelson Mandela amekimbizwa tena hospitali kupatiwa matibabu ya mapafu, ugonjwa ambao umeambata na matatizo ya kupumua, ikulu ya nchi hiyo imethibitisha. 

Mzee Nelson Mandela akitolewa hospitali akiwa kwenye kitanda hivi karibuni
Mzee Nelson Mandela akitolewa hospitali akiwa kwenye kitanda hivi karibuni Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mandela ambaye sasa ana umri wa miaka 94 amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwenye miaka ya hivi karibuni ambapo mara kadhaa alikimbizwa hospitali kwa matibabu ya maradhi kama hayo ambayo madaktari wanasema yanatokana na uzee.

Mzee Mandela anakimbizwa hospitalini ikiwa mepita miezi kadhaa toka atoke hospitalini kupatiwa matibabu ya mapafu ambapo msemaji wa ikulu aliwahakikishia wananchi kuwa muasisi huyo anaendelea vizuri.

Mzee Nelson Mandela ambaye alikuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi wakati wa utawala wa kikoloni na wakati fulani akijikuta akihukumiwa kifungo cha maisha ameendelea kuwa nembo ya taifa hilo kwa harakati za kimapinduzi.

Hofu imetanda nchini humo kuhusu afya ya kiongozi huyo ambapo ikulu ya rais Zuma imetoa wito kwa wananchi na dunia kwa ujumla kumuombea kiongozi huyo ambaye afya yake inaelezwa kuzorota.

Madaktari wanaomtimu mzee Mandela wamesema wanaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha waampatia huduma bora zaidi na zajuu kunusu maisha ya kiongozi huyo.

Rais Jackob Zuma ambaye ametumia jina la kimila la mzee Mandela kama “Madiba” amemtakia heri kiongozi pamoja na familia yake katika kipindi hiki kigumu ambacho mzee Madiba anapitia.