SYRIA-UN

UN: Waangalizi wetu bado hawajaruhusiwa kuingia nchini Syria kufanya uchunguzi wa silaha za kemikali

Serikali ya Syria bado haijatoa kibali kwa waangalizi wa Umoja wa Mataifa UN, kuingia nchini humo kutembelea maeneo ambayo yanadaiwa kuwa pande hizo mbili zinazopiganan nachini humo zimekuwa zikitumia silaha za kemikali. 

Moja ya majengo ambayo yameharibiwa kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Syria
Moja ya majengo ambayo yameharibiwa kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Syria Reuters/Hamid Khatib
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa UN kupitia baraza la usalama waliidhinisha kupelekwa kwa wachunguzi wake nchini Syria kukagua iwapo tuhuma za kuwa wapoganaji wa Syria na vile vikosi vya Serikalo vimekuwa vikitumia silaha za kemikali kwenye uwanja wa mapambano.

Hatua hiyo ya Umoja wa Mataifa inakuja kufuatia ripoti ya mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Syria kudai kuwa wanaushahidi unaoonesha kuwa wanajeshi huru wa Syria na wale wa Serikali wamekuwa wakikabiliana kwa kutumia silaha za Kemikali ambazo zinakatazwa kimataifa.

Pande zote mbili zimekuwa zikitupiana lawama kuwa kila upande unatumia silaha za kemikali jambo ambalo limezusha hofu ya kiusalama kwa wananchi na hata jumuiaya ya kimataifa iwapo ni kweli silaha hizo zinatumika.

Timu ya wataaalamu wa Umoja huo wanatakiwa kuanza kazi mapema wiki ijayo lakini mpaka sasa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kati ya upande wa Serikali ya rais Asad kuhusu namna ambavyo uchunguzi huo utafanyika.

Serikali ya Syria ndio iliyoutaka Umoja wa Mataifa UN kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo ya kwamba wapiganaji wa jeshi huru la Syria walitumia silaha za Kemikali kwenye mji wa Allepo dhidi ya vikosi vya rais Asad.

Siku ya Jumanne katibu mkuu wa Umoja huo, Ban Ki Moon, alimtangaza Ake Sellstrom raia wa Sweeden kuongoza timu ya wataalamu wa Umoja huo kwenye nchini Syria kufanya uchunguzi