DRC-UN

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laidhinisha kupelekwa kwa kikosi maalumu cha kulinda amani nchini DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC kwa mara ya kwanza limeidhinisha Kikosi cha Kulinda Amani kupelekwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambapo kimepewa mamlaka ya kukabiliana na Makundi ya Waasi tofauti na ilivyokuwa kabla. Azimio hilo ambalo linakipa mamlaka Kikosi hicho chenye wanajeshi elfu tatu kuweka hali ya utulivu sambamba na kuyanyang'anya silaha Makundi yote ambayo yanashikilia zana hizo za kivita na kutela hofu ya usalama. 

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani mjini Katanga, UN imeidhinisha kupelekwa kwa vikosi zaidi
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani mjini Katanga, UN imeidhinisha kupelekwa kwa vikosi zaidi UN Photo/Myriam Asmani
Matangazo ya kibiashara

Kikosi hicho kitakuwa tayari kufanyakazi na Majeshi ya Tanzania, malawi na Afrika Kusini yanayotarajiwa kuelekea Mashariki mwa DRC ambapo Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous anasema hatua hiyo ni muhimu kwa mustakabali wa wananchi wa DRC.

Vikosi hivyo vinatarajiwa kuweoo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa muda wa mwaka mmoja lakini kuna uwezekano pia muda huo ukaongezwa kulingana na majukumu ambayo majeshi hayao yatakuwa nayo pamoja na hatua ambazo zitakuwa zimefikiwa kuwakabilia waasi.

Baraza la Usalama pia limeruhusu kutumika kwa ndege maalumu zisizo na rubani katika maeneo ya mpakani mwa nchi hiyo ndege ambazo awali nchi ya Rwanda ilipinga kutumika kwa kile ilichoeleza ni kushindwa kwa ndege hizo kule nchini Pakistan.

Operesheni nchini DRC imedhaminiwa na nchi za Ufaransa, Marekani na Togo ambazo zitahakikisha kikosi hicho mbali na kuwalinda wananchi dhidi ya uasi wa kundi la M23, pia kitakuwa na jukumu la kulinda usalama wa taifa ili kukabiliana a hatari zozote zitakazotishia Serikali halali ya nchi hiyo.

Kwa pamoja wajumbe wa UNSC wamelaani uwepo wa waasi wa M23 kwenye mji wa Goma na maeneo ambayo wanayashikilia wakiwataka waasi hao kuanza kujisalimisba wenyewe kwa wanajeshi wa Serikali kabla ya kukukabiliana na nguvu ya Jumuiya ya Kimataifa.