Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Muungano wa Seleka unaendelea kuhaha kurejesha hali kama ilivyokuwa kabla ya Mapinduzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kipindi hiki Cyprus ikipitia kwenye mdororo wa uchumi uliochangia kuzuka kwa maandamano

Imechapishwa:

Utawala mpya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati chini ya Uongozi wake Mkuu wa Muungano wa Seleka Michel Djotodia unaendelea kuhakikisha hali inarejea kama ilivyokuwa kabla ya kufanyika kwa Mapinduzi nchini humo na kuanguka kwa Serikali ya Rais Francois Bozize, Umoja wa Mataifa UN kupitia Baraza la Usalama la Umoja huo umeamua kulivalia njuga suala la amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokarsia ya Congo DRC na sasa inapeleka Kikosi ambacho kitakabiliana na Makundi yanayomiliki silaha na Hatimaye nchi ya Cyprus imepata ahueni baada ya kupewa mkopo wa dola bilioni kumi kutoka Umoja wa Ulaya EU na Shirika la Fedha Duniani IMF ili kukabiliana na kudorora kwa uchumi wa Taifa hilo!!

Kiongozi wa Muungano wa Seleka aliyejitangaza Rais, Michel Djotodia akiwa na Rais aliyepinduliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize
Kiongozi wa Muungano wa Seleka aliyejitangaza Rais, Michel Djotodia akiwa na Rais aliyepinduliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize AFP PHOTO / STEVE JORDAN
Vipindi vingine