Habari RFI-Ki

Waasi wa M23 Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wapinga hatua ya Umoja wa Mataifa UN kupeleka Kikosi Maalum Mashariki mwa Taifa hilo

Sauti 09:56
Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 wakiwa katika Mji wa Goma lakini sasa watakabiliwa na upinzani kutoka kwa Jeshi Maalum la Umoja wa Mataifa UN
Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 wakiwa katika Mji wa Goma lakini sasa watakabiliwa na upinzani kutoka kwa Jeshi Maalum la Umoja wa Mataifa UN REUTERS/Goran Tomasevic

Kundi kubwa la Waasi linalopatikana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC M23 limejitokeza na kupinga kwa nguvu zake hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC kupitisha azimio la kupeleka Jeshi Maalum litakalopambana na Makundi ya Waasi yanayopatikana katika eneo hilo na si kulinda amani pekee kama ilivyokuwa imezoeleka.