Mjadala wa Wiki

Mahakama Kuu nchini Kenya yausafisha ushindi wa Rais Mteule Uhuru Muigai Kenyatta na kuzima kesi ya Raila Odinga

Sauti 12:36
Majaji Sita wa Mahakama Kuu nchini Kenya wakiongozwa na Jaji Mkuu Dr Willy Mutunga kabla ya kutoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi
Majaji Sita wa Mahakama Kuu nchini Kenya wakiongozwa na Jaji Mkuu Dr Willy Mutunga kabla ya kutoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi

Jumamosi iliyopita Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya waliafikiana kwa pamoja kuwa Rais Mteule Uhuru Muigai Kenyatta alishinda kihalali uchaguzi wa urais nchini humo mwezi uliopita. Uhuru Kenyatta sasa ataapishwa siku ya Jumanne juma lijalo jijini Nairobi. Waziri Mkuu Raila Odinga aliyewasilisha kesi Mahakamani Kuu kupinga ushindi huo tayari amekiri kukubaliana na uamuzi wa mahakama na kuwapongeza wapinzani wake.