Habari RFI-Ki

Msako wa Kiongozi wa Kundi la Waasi la LRA Joseph Kony waongezewa nguvu baada ya Marekani kutanga dau la Dola Milioni 5

Sauti 10:22
Kiongozi wa Kundi la Waasi la LRA Joseph Kony anayesakwa huku donge nunu likitolewa kufanikisha kukamatwa kwake
Kiongozi wa Kundi la Waasi la LRA Joseph Kony anayesakwa huku donge nunu likitolewa kufanikisha kukamatwa kwake

Serikali ya Marekani imetangaza zawadi ya dola milioni tano kwa yoyote ambaye atafanikisha kukamatwa kwa Kiongozi wa Kundi la Waasi la Lord's Resistance Army LRA Joseph Kony anayesakwa kwa udi na uvumba. Serikali ya Marekani imeamua kutangaza zawadi hiyo kutokana na operesheni za kumsaka Kony kuonekana kugongwa mwamba huku Uganda wakitangaza kusitisha msako waliokuwa wanaufaya kwa muda.