Habari RFI-Ki

Wabunge Nchini Kenya waanza mchakato wa kutaka kuongezewa mishahara kabla ya kuanza kibarua chao juma lijalo

Sauti 09:55
Bunge la Kenya ambalo linatumiwa na Wabunge wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi Barani Afrika
Bunge la Kenya ambalo linatumiwa na Wabunge wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi Barani Afrika

Wabunge nchini Kenya wanatarajiwa kuanza kazi mapema juma lijalo lakini tayari wameshaanza mkakati wa kutaka kupatiwa nyongeza ya mshahara. Hatua hiyo inakwenda kinyume na Kamati Inayohusika Kurekebisha Mishahara imeshapanga viwango vya mishahara kwa Maseneti na Wabunge. Hatua hiyo haijawaridhisha kabisa wabunge na wameanza kuweka mpango wa kuongezewa mshahara.