Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Tanzania yatangaza msimamo wao juu ya mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa na Jirani zao Malawi huku hofu ya kuzuka vita kati ya Korea Kaskazini na Marekani ikizidi kukua

Sauti 20:39
Pwani ya Ziwa Nyasa inayosababisha nchi jirani za Tanzania na Malawi kuingia kwenye mgogoro wa mpaka
Pwani ya Ziwa Nyasa inayosababisha nchi jirani za Tanzania na Malawi kuingia kwenye mgogoro wa mpaka

Makala haya juma hili yatajikita kuangalia masuala matatu makubwa yaliyogonga vichwa vya habari ambayo ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa msimamo wake juu ya mgogoro wa mpaka na Malawi, Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Kati ECCAS kukutaa kuitambua serikali ya Seleka na Hofu ya kuibuka vita vya tatu vya dunia vitakavyochochewa na Marekani pamoja na Korea Kaskazini.