Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Uhuru Muigai Kenyatta aapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Kenya na Wananchi wa Uingereza waomboleza kifo cha Waziri Mkuu wa Kwanza Mwanamke Margareth Thatcher

Sauti 21:20
Rais wa Awamu ya Nne wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta akila kiapo cha kuongoza nchi hiyo baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika tarehe 4 Machi
Rais wa Awamu ya Nne wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta akila kiapo cha kuongoza nchi hiyo baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika tarehe 4 Machi

Uhuru Muigai Kenyatta aapishwa kushikwa wadhifa wa Urais wa nne katika Jamhuri ya Kenya pamoja na Naibu Rais William Samoei Arap Ruto katika sherehe ambazo zimehudhuriwa na Marais kumi kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika, Waasi wa Kundi la M23 linalopambana na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wamerejea kwenye mazungumzo huku wakiandamwa na mzimu wa kupelekwa kwa Kikosi Maalum kutoka Umoja wa Mataifa UN kupambana na Makundi ya Waasi huko Mashariki na Wananchi wa Uingereza waendelea kuomboleza kifo cha Waziri Mkuu wa Kwanza Mwanamke Margareth Thatcher ambaye alihudumu kwa kipindi cha miaka kumi na moja!!