MAREKANI-BOSTON

FBI yabaini kifaa kilichotumiwa kutekeleza mashambulizo ya bomu

Uchunguzi wa awali unaofanywa na shirika la ujajusi nchini Marekani FBI umeonesha mabomu yaliyotumiwa kutekeleza mashambulizi katika mstari wa kumalizia mbio ndefu mjini Boston siku ya Jumatatu na kusababisha vifo vya watu watatu na mamia kujeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Picha za mabomu hayo zinaonesha kuwa kifaa kilichotumiwa kutekeleza mashambulizi hayo inashukiwa kuwa mtambo wa kupikia uliotumiwa kutengeza mabomu hayo.

Mitambo iliyopatikana imetumwa katika maabara ya Quantico, katika jimbo la Virginia kuzichunguza zaidi ili kutolewa kwa maelezo ya kina kuhusu shambulizi hilo.

Rais Barrack Obama atakuwa mjini Boston siku ya Jumatano kuhudhuria ibada ya kuwaombea waliouamia na kuombeleza na familia ya watu watatu waliopoteza maisha yao.

Aidha, Obama amesema kuwa lazima waliotekeleza mashambulizi hayo wachukuliwe hatua za kisheria, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akilaani tukio hilo.

Shambulizi la kwanza lilitokea saa mbili baada ya washindi kuvuka mstari wa mwisho huku polisi wakiwa na wakati mgumu kuwasaidia wale waliokumbwa na milipuko hiyo.

Polisi mjini Boston wametoa wito kwa wakaazi wa mji huo kuepuka mikusanyiko ya watu wakati huu ambao bado hali ya usalama si ya kuridhisha kutokana na mashambulizi hayo.

Miaka kumi iliyopita mashambulizi ya mabomu yalisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu tatu  mjini New York,Washington DC  na Pennsylvania.