Nyumba ya Sanaa

Kumbukumbu ya mwaka mmoja baada ya kifo cha msanii Steven Kanumba na Kifo cha msanii mkongwe nchini Tanzania Bi. Kidude

Sauti 20:07

Makala ya Nyumba ya Sanaa juma hili inaangazia kifo cha msanii mkongwe wa muziki wa taarabu nchini Tanzania Fatma Binti Baraka maarufu kwa jina la Bi. Kidude, pia utapata kusikia maswala mbalimbali yaliyojiri katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha msanii wa filamu wa nchini Tanzania Steven Charles Kanumba. Ungana na mtayarishaji wa makala haya Edmond Lwangi Tcheli akiwa na mtangazaji mwingine wa rfi kiswahili Emmanuel Makundi, karibu.