Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Wabunge Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC waonesha kutokuwa na imani na Serikali huku Marekani ikishuhudia milipuko Boston na Texas

Sauti 20:08
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Joseph Kabila wa Kabange ambaye serikali yake imepigiwa kura ya kutokuwa na imani nayo
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Joseph Kabila wa Kabange ambaye serikali yake imepigiwa kura ya kutokuwa na imani nayo Reuters/Tiksa Negeri

Wabunge nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC juma hili walioneshwa kutokuwa na imani na serikali ya Rais Joseph Kabila wa Kabange na hivyo wakafikisha hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani iliyoshindwa, Kundi la Wanamgambo wa Al Shabab lenye maskani yake nchini Somalia limeanza kuonesha tena umahiri wake baada ya juma hili kutekeleza shambulizi na kusababisha vifo huko Mogadishu na Serikali ya Marekani inaendelea kuhaha kuhakikisha usalama unaimarika katika taifa hilo baada ya kushuhudia milipuko huko Boston na mwingine kwenye Kiwanda cha Mbolea Mjini Texas!!