Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mawaziri Wateule wa Baraza la Mawaziri wa Kenya watajwa huku Serikali ya Syria ikiingia lawamani kwa kutumia silaha za kemikali

Sauti 19:39
Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta akiwa na Naibu Wake William Samoei Ruto wakitaja majina ya Mawaziri Wateule
Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta akiwa na Naibu Wake William Samoei Ruto wakitaja majina ya Mawaziri Wateule

Majina ya Mawaziri Wateule kumi na sita watakaounda Baraza la Mawaziri lenye Mawaziri kumi na wanane nchini Kenya yametangazwa huku mjadala ukizuka kutokana na kutajwa kwa wanasiasa wawili wa zamani katika orodha hiyo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC limeridhia hatua ya kupeleka Wanajeshi wa Kulinda Amani nchini mali kuhakikisha wanaweka hali ya utulivu baada ya kumalizika kwa operesheni ya kuyasambaratisha Makundi ya Kiislam na Serikali ya Syria yatuhumiwa kutumia silaha za kemikali kwenye mapambano yao dhidi ya Wapiganaji wa Upinzani wanaotaka kung'oa madarakani Utawala wa Rais Bashar Al Assad!!