Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Kundi la Waasi la M23 la Nchini DRC lapata pigo baada ya Maafisa wake wa Kijeshi kuasi huku Msuluhishi wa Mgogoro wa Syria Lakhdar Brahimi akitangaza kubwaga manyanga

Sauti 21:38
Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 wakiwa katika Mji wa Goma walipouteka kwa mara ya kwanza
Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 wakiwa katika Mji wa Goma walipouteka kwa mara ya kwanza REUTERS/Goran Tomasevic

Waasi wa M23 wa Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wameanza kudhoofika baada ya Maafisa wao wa Ngazi ya juu ya Kijeshi kutangaza kuasi na kujisalimisha kwenye Makao Makuu ya Vikosi vya Kulinda Amani MONUSCO, Wananchi Duniani kote jumatano hii waliadhimisha Siku ya wafanyakazi ambapo changamoto imeendelea kuwa ukosefu wa ajira pamoja na malipo madogo na Msuluhishi wa Mgogoro wa Syria Lakhdar Brahimi hatimaye amesalimu amri na kutangaza kujiuzulu wadhifa wake mwishoni mwa mwezi May kutokana na kushindwa kufikia malengo yake ya kurejesha usalama!!