Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewakamata watu kumi na wawili wakihusishwa na shambulizi la bomu Arusha huku Mataifa 50 yakikutana Uingereza kusaka mbinu za kuisaidia Somalia

Sauti 20:10
Waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi wakikimbia ovyo baada ya kutokea shambulizi la kujitoa mhanga kanisani hapo
Waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi wakikimbia ovyo baada ya kutokea shambulizi la kujitoa mhanga kanisani hapo

Jeshi la Polisi nchini Tanzania linawashikilia watuhumiwa kumi na wawili wanaotajwa kuhusika kutekeleza shambulizi la bomu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti Mkoani Arusha, Viongozi kutoka mataifa 50 wamekutana nchini Uingereza ikiwa ni sehemu ya kusaka mbinu za kuisaidia Somalia iweze kujijenga upya baada ya kupitia kwenye vita kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili na Upinzani nchini Syria waingia matatizoni baada ya kudaiwa kutumia silaha za kemikali kwenye vita vyao dhidi ya Jeshi la Serikali licha ya kuwa mataifa ya Magharibi yamepinga taarifa hizo!!