Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Vyombo vya Habari nchini Uganda vimepata pigo baada ya Serikali kuvifungua vinne kipindi hiki Serikali ya Uingereza ikisema walimuua mwanajeshi wake ni magaidi

Imechapishwa:

Nchini Uganda Vyombo vya habari nchini humo vimefungwa na Jeshi la Polisi linalofanya msako wa kutaka kupata nyaraka zinazotaja uwepo wa njama za kutaka kuuawa kwa Viongozi wa Kijeshi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejiapiza kuhakikisha inawashughulikia wale wote ambao wanachochea kuzuka kwa ghasia Mkoani Mtwara kwa kisingizio cha kupinga kujengwa kwa bomba la gesi kuelekea Dar Es Salaam, Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC mapigano yameendelea kushuhudiwa kati ya Jeshi la FARDC na Waasi wa M23 kipindi hiki Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amezulu Goma na kuahidi usalama utarejea na Nchini Uingereza watu wawili wanatuhumiwa kutekeleza mauaji ya mwanajeshi wa Taifa hilo tukio ambalo Serikali imelita la kigaidi na si kidini!!

Polisi nchini Uganda wakiwa wamezifunga ofisi za Gazeti la Daily Monitor zilizopo katika eneo la Namuwongo, Kampala
Polisi nchini Uganda wakiwa wamezifunga ofisi za Gazeti la Daily Monitor zilizopo katika eneo la Namuwongo, Kampala
Vipindi vingine