Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Viongozi wa nchi za Afrika wageuka mbogo na kuishutumu Mahakama ya ICC kuwa ya kibaguzi huku Mgogoro wa Syria ukiendelea kuchukua sura mpya

Sauti 21:17
Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 tangua kuanzishwa kwake sherehe zilizofanyika Mjini Addis Ababa
Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 tangua kuanzishwa kwake sherehe zilizofanyika Mjini Addis Ababa

Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU wamefanya maadhimisho ya miaka hamsini tangu kuanzishwa kwa umoja wao huku wakianzisha mapambano mapya dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC kwa kuwafungulia mashtaka viongozi wa bara hilo pekee, Juhudi za kusaka zuluhu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC zimeendelea kipindi hiki Kikosi Maalum cha Umoja wa Mataifa UN kikisubiriwa kwa hamu kubwa na Machafuko nchini Syria yachukua sura mpya baada ya Urusi kuwapatia wanajeshi wa Rais Bashar Al Assad silaha wakijibu uamuzi wa Umoja wa Ulaya EU kutoa silaha kwa Upinzani!!