Mjadala wa Wiki

Rasimu ya Katiba Mpya nchini Tanzania yaendelea kupongezwa kutokana na mapendekezo yaliyoorodheshwa ndani

Sauti 14:53
Makamu wa Rais wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilal akionesha rasimu ya katiba mpya akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Joseph Sinde Warioba
Makamu wa Rais wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilal akionesha rasimu ya katiba mpya akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Joseph Sinde Warioba

Wataalam wa Masuala ya Sheria na Siasa wamekuwa ni miongoni mwa wale waliopongeza mapendekezo yaliyowekwa kwenye rasimu ya katiba ya mpya ya Tanzania ambayo imeweza kupendekeza uwepo wa Serikali tatu pamoja na kuliweka kando suala la Mahakama ya Kadhi. Wataalam hao wamekiri kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesaidia kupatikana kwa rasimu nzuri inayoweza kusaidia kupatikana kwa katiba nzuri!!