Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mgawanyiko waanza kulinyemelea Taifa la Misri kutokana na uwepo wa maandamano huku Urusi ikiwasilisha ushahidi kuonesha Waasi nchini Syria unatumia silaha za kemikali

Sauti 20:03
Wafuasi wa Kiongozi aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohamed Morsi wakiendelea na maandamano yao kushinikiza arejeshwe madarakani
Wafuasi wa Kiongozi aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohamed Morsi wakiendelea na maandamano yao kushinikiza arejeshwe madarakani REUTERS/Suhaib Salem

Hofu imeanza kutanda nchini Misri huenda nchi hiyo ikaingia kwenye mgawanyiko mkubwa kutokana na upinzani unaoendelea kukita mizizi baina ya Wafuasi wa Mohamed Morsi na wale ambao wanampinga Kiongozi huyo kwenye uhasama mkubwa unaoambatana na maandamano, Mwanga wa kupatikana kwa usalama na amani ya kudumu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC waanza kuonekana kufuatia Kundi la Waasi la M23 na Ujumbe wa Serikali ya Kinshansa kuwa njiani kusaini makubaliano ya kumaliza mapigano na Urusi imewasilisha ushahidi wa kudhihirisha Waasi nchini Syria ndiyo vinara wa kutumia silaha za kemikali kitu ambacho kimepingwa vikali na Marekani!!