ISRAEL-IRAN-MAREKANI

Israel yatishia kuishambulia Iran iwapo itaendelea na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia

Waziri mkuu wa Uingereza, Benjamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Uingereza, Benjamin Netanyahu Reuters

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema nchi ya Iran inakaribia kabisa kukamilisha kutengeneza silaha za nyuklia na kwamba nchi yake italazimika kuchukua hatua mapema kabla ya nchi hiyo kumiliki silaha kali.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu Netanyahu ameongeza kuwa Tehran inakaribia kabisa kuvuka mstari mwekundu alioiwekea japo bado haijavuka lakini kuna kila dalili kuwa taifa hilo litavuka mstari huo na Israel italazimika kujihami.

Waziri mkuu huyo akongeza kuwa nchi ya Israel haina mjadala katika hili ukilinganisha na nchi ya Marekani ambayo imeendelea kuitazama serikali ya Tehran ikiendelea na mpango wake wa kutengeneza bomu la Nyuklia.

Nchi ya Israel mara zoet imekuwa ikiituhumu nchi ya Iran kuwa na mpango wa kutengeneza bomu la Nyuklia ambalo huenda likatumika kuivamia nchi yake jambo ambalo waziri mkuu Netanyahu anasema kamwe hataliacha litokee.

Ameongeza kuwa sera ya nchi ya Iran kuhusu nyuklia huenda isibadilike licha ya kuingia madarakani kwa rais mpya Hassan Rowhani ambaye alitangaza kuwa atafanya mazungumzo na nchi za magharibi kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Waziri Netanyahu amemtuhu rais anayemaliza muda wake, Mahmoud Ahmadineijad kwa kuwa alikuwa mkaidi katika kuruhusu waangalizi wa Umoja wa Mataifa UN kuingia nchini humo kufanya uchunguzi kwenye vinu vyake.