UGANDA-DRC-ADF-NALU

Jeshi la Uganda lakiri wapiganaji wa ADF-NALU wanapatiwa mafunzo na kundi la Al-Shabab

Msemaji wa jeshi la Uganda, Luteni kanali, Paddya Ankunda
Msemaji wa jeshi la Uganda, Luteni kanali, Paddya Ankunda Reuters

Jeshi la Uganda limesema wapiganaji waasi wa ADF -NALU wanaopigana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wanapatiwa mafunzo na wanamgambo wa Al-Shabab.   

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Uganda, Paddya Ankunda amedhibitisha jeshi lao kuwa na taarifa kuhusu mafunzo yanayotolewa na Al-Shabab kwa wapiganaji wa ADF-NALU ambao katikati ya juma lililopita walianzisha uasi mashariki mwa DRC.

Taarifa ya Jeshi la Uganda inatolewa saa chache baada ya Serikali ya DRC nayokukiri kuwashuhudia wapoganaji wakiislamu mashariki mwa nchi hiyo ambao wamekuwa wakishirikiana na waasi wa M23 ambao wanaipinga Serikali ya Kinshasa.

Tayari jeshi la Uganda limetangaza kuwa katika hali ya tahadhari kufuatia mapigano ya DRC na kwamba limejiandaa kukabiliana na waasi wa ADF _NALU iwapo watajaribu kuingia nchini humo.

Katika hatua nyingine shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limesema zaidi ya raia elfu 55 roka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRc wameikimbia mapigano.

Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu nchini Uganda, Catherine Ntabadde amesema kila siku kumekuwa na ongezeko kubwa la wakimbizi kwenye kambi ya Bundibugyo iliyoko mpaka na nchi ya DRC.

Siku ya Alhamisi wananchi wa mji wa Kamango nchini DRC walijikuta kwenye mapigano baada ya wapiganaji waasi wa Uganda, ADF-NALU kuvamia eneo hilo na kulishikilia.

Mapigano haya yazuka wakati huu ambapo vikosi maalumu vya Umoja wa Mataifa UN, viko mashariki mwa DRC kwa lengo la kukabiliana na makundi ya waasi ambao wamekuwa wakizorotesha usalama kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Wachambuzi wa mambo wanahoji ni lini vikosi hivyo vitaanza kufanya kazi ya kukabiliana na makundi hayo wakati huu ambapo maelfu ya raia wanaendelea kuikimbia nchi yao.