MISRI

Mkuu wa majeshi ya Misri atetea uamuzi wa jeshi kumng'oa madarakani Mohamed Morsi

Jenerali Abdel al-Sisi akiwa na rais Morsi kabla ya kutangaza kumuondoa madarakani
Jenerali Abdel al-Sisi akiwa na rais Morsi kabla ya kutangaza kumuondoa madarakani Reuters

Mkuu wa majeshi ya Misri, ametetea uamuzi wa jeshi la nchi hiyo kuingilia kati mzozo wa kisiasa uliuokuwa unafukuta na hatua ya kumuondoa madarakni rais Mohamed Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood.

Matangazo ya kibiashara

Jenerali Abdel-Fattah al-Sisi amesema kuwa rais Morsi alivuka mipaka ya madaraka yake na kukiuka sheria halali za nchi na kuiweka rehani katiba ya nchi hiyo ambayo ilipaswa kuwa muongozi wake wa kuongoza Serikali.

Jenerali al-Sisi ameongeza kuwa rais Morsi aliingia kwenye mgogoro na mahakama, vyombo vya habari, polisi na kupinga maoni ya watu ambao ndio waliompigia kura kumuweka madarakani na zaidi akaingilia mamlaka ya jeshi.

Wakati wa hotuba yake hakuweka wazi mgogoro kati ya jeshi na Serikali yake lakini kitendo cha kulidharau jeshi na kusema kwamba halina mamlaka ya kuingia sias za nchi hiyo hataka kama nchi inaingia kwenye machafuko ni kukiuka katiba ya nchi.

Akizungumzia hatua walizochukua kabla ya kumuondoa madarakani rais Morsi, Jenerali al-Sisi amesema aliwasiliana na Morsi na kumshauri namna ya kusuluhisha mgogoro huo kabla ya kumpa saa 48 ambazo hata hivyo rais Morsi hakutaka kufanyia kazi ushauri wake.

Kiongozi huyo wa kijeshi amezitaka pande zote kushiriki kwa mazungumzo ya kitaifa kutafuta suluhu ya kisiasa nchini humo kuliko kuendelea na maandamano ambayo hayana tija kwasasa.

Katika hatiua nyingine mwendesha mashtaka wa Serikali ametangaza kuanzisha ushunguzi dhidi ya rais Morsi kuhusu kukiuka katiba ya nchi na matumizi mabaya ya ofisi akiwa kiongozi wa nchi.

Wakati huohuo maofisa wa Serikali ya Marekani wamewasili mjini Cairo kwa mazungumzo na Serikali ya mpito kuangalia namna ya kumaliza mzozo wa nchi hiyo.