MAREKANI-FLORIDA

Mwanasheria wa Marekani aingilia kati sakata la kesi dhidi ya Zimmerman aliyeachiwa huru juma hili

Mwanasheria wa Serikali ya Marekani, Eric Holder
Mwanasheria wa Serikali ya Marekani, Eric Holder Reuters

Mwanasheria mkuu wa Serikali ya Marekani, Eric Holder amesema kuwa uchunguzi dhidi ya mauaji ya Trayvone Martin utaendelea licha ya mahakama mjini Florida kumkuta hana hatia George Zimmerman.

Matangazo ya kibiashara

Holder amesema kuwa kifo cha Martin kilikuwa kinaepukika na kwamba Zimmerman licha ya kuwa alijihami lakini angeweza kutoa nafasi ya kuishi kwa kijana huyo kwa kumjeruhi na risasi maeneo mengine ya mwili.

Ofisi ya mwendesha mashataka wa Serikali ilifungua kesi dhidi ya Zimmerman mwaka jana lakini baadae ilijitoa na kumwachia mwendesha mashtaka wa Florida aendelee na kesi hiyo ambayo juma hili ndio imetolewa uamuzi.

Mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, kumeshuhudiwa maandamano nchi nzima ambapo wanaharakati na wananchi wanapinga kuachiwa kwa Zimmerman kwa kile wanachodai anapaswa kuwajibishwa kutokana na mauaji ya Martin.

Wakati wa kesi yake Zimmerman ameendelea kusisitiza kuwa hakuwa na jinsi wakati alipovamiwa na kijana huyo na kwamba alijihami kwa kumpiga risasi ambayo hata hivyo ilikatisha uhai wa kijana mwenye umri wa miaka 17.

Baadhi ya wanasheria pia wamehoji mfumo wa sheria za Marekani ambao mara nyingi zimekuwa zikiishia kuwaachia huru watuhumiwa wa mauaji kwasababu ya kuwa zinaruhusu mtu kujihami kwa silaha yoyote na hata ikiwezekana kuua.

Hatua ya mwanasheria wa serikali kutangaza kuingilia kati sakata hilo kumeelezwa ni muhimu kufanya hivyo kwasasa kwakuwa wanaweza kufungua kesi ya kuua bila kukusudia na hatimaye kumkuta na hatia Zimmerman ambaye sasa yuko huru.