DRC

Wapiganaji 120 wa M23 wauawa mashariki mwa DRC, huku maelfu ya raia wakiendelea kukimbia makazi yao

Reuters

Mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali ya DRC na waasi mashariki mwa nchi hiyo yamesababisha vifo vya watu 130 wakiwemo wanajeshi kumi, taarifa ya Serikali ya DRC imesema. 

Matangazo ya kibiashara

Idaidi hiyo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika mwezi mmoja pekee kati ya waasi wanaoshikilia maeneo ya mashariki mwa mji wa Goma na wanajeshi wa Serikali ya DRC.

Milio ya risasi na mabomu imesikika kwenye mji wa Goma usiku wa kuamkia leo ambapo inakadiriwa kuwa watu zaidi ya elfu moja wamekimbia makazi yao kuhofia maisha yao.

Msemaji wa jeshi la Serikali ya DRC, Lambert Mende amesema jeshi la Serikali limefanikiwa kuwaua wapiganaji wa M23 120 na kuwakamata waasi wengine kumi na mbili ambao walijisalimisha kwa hiari yao.

Mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali na waasi wa M23 yalizuka siku ya Jumapili kwenye jimbo la Kivu ya Kaskazini ambalo linautajiri mkubwa wa madini ambayo hutumika kutengeneza vifaa vya simu na vifaa vingine vya umeme.

Serikali ya DRC imeendelea kuituhumu Serikali ya Rwanda kwa kuendelea kuwafadhili waasi wa M23 ambao wameendelea kujikusanya mashariki mwa nchi hiyo huku wakijibu mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Serikali.

Vikosi maalumu vya Umoja wa Mataifa UN vilivyoko mashariki mwa nchi hiyo bado havijaanza kazi rasmi ya kukabiliana na makundi ya waasi ambapo wanachofanya sasa ni kukusanya silaha ambazo zinasalimishwa na waasi.

Katika hatua nyingine, maelfu ya wananchi wa DRC wameendelea kukimbia nchi yao na kuingia nchini Uganda kuomba hifadhi kutokana na kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano kati ya Serikali na waasi wa ADF-NALU.

The M23, an armed group launched by Tutsi former soldiers who mutinied from the Congolese army in April 2012, blamed the government for the fighting.