MISRI

Baraza jipya la mawaziri laapishwa nchini Misri, Muslim Brotherhood wasema hawalitambui baraza hilo

Baraza jipya la Misri likiwa kwenye picha ya pamoja
Baraza jipya la Misri likiwa kwenye picha ya pamoja Reuters

Rais wa mpito wa Misri ameliapisha baraza lake jipya la mawaziri huku akiwapa nafasi viongozi wenye msimamo wa kati na pia akiwajumuisha wanawake wawili kwenye Serikali mpya. Serikali mpya inaongozwa na waziri mkuu, Hazem el-Beblawi ambaye kwa taaluma ni mchumi, Abdel-Fattah al-Asisi ambaye ataendelea kushikilia nafasi yake ya waziri wa ulinzi na pia Kama naibu waziri mkuu wa kwanza.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa masuala ya ndani ambaye aliteuliwa na rais aliyepinduliwa, Mohamed Ibrahim ataendelea kushikilia wadhifa wake, huku Nabil Fahmy ambaye aliwahi kuwa balozi wa Misri nchin Marekani, sasa atakuwa Kama waziri wa mambo ya nje.

Akisisitiza kwanini baraza lake limejumuisha viongozi wenye msimamo wa Kati, rais wa mpito, Adly Mansour amesema amazingatia mahitaji ya nchi huku akitangaza nafasi tatu za wanawake kwenye baraza lake.

Wizara walizopewa wanawake hao ni pamoja na wizara ya habari, wizara ya afya na wizara ya mazingira, uteuzi ambao unaonekana haukutarajiwa na wananchi wengi.

Baraza Hilo jipya lina jumla ya mawaziri thelathini na wanne huku waziri mkuu el-Beblawi akiwajumuisha hajajumuishwa kwakuwa ni waziri mkuu tayari.

Hata hivyo baraza hili jipya lililotangazwa na rais Mansour limeonekena kawa la tofauti kutokana na viongozi wengi waliotangulia kujumjisha wanawake wasiozidi wawili kwenye mabaraza Yao.

Hata hivyo uteuzi wa mawaziri hao haujajumuisha kiongozi yeyote wa juu toka vyama vya kiislamu huku msemaji wa rais akisema nafasi nyingine wamewekewa viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood.

Punde Mara baada ya kutangazwa kwa baraza na kuapishwa, viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood wamesema hawatashiriki kwenye Serikali ambayo imeingia madarakani kwa kutumia nguvu za kijeshi na kuapa kufanya maandamano zaidi.

Wafuasi wa Muslim Brotherhood wanalikosoa jeshi la nchi hiyo kwa kuipindua Serikali halali na kuharibu demokrasia ya Misri.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kawa baraza hilo sio jipya sana kwakuwa karibu mawaziri saba waliokuwa kwenye Serikali iliyoangushwa wameendelea kushikilia nyadhifa zao.

Msemaji wa chama cha Muslim Brotherhood, Gehad El-Haddad amelikashifu baraza hilo akisema ni batili na halina mamlaka ya utawala kwakuwa hata Serikali yenyewe haijachaguliwa kidemokrasia.