ZIMBABWE

Tsvangirai: Sina imani tena na tume ya taifa ya uchaguzi ya Zimbabwe, ZEC

Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai ambaye pia ni kiongozi wa upinzani
Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai ambaye pia ni kiongozi wa upinzani REUTERS/Philimon Bulawayo

Waziri mkuu wa Zimbabwe ambaye pia ni kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo amesema amekosa imani na tume ya taifa ya uchaguzi ZEC kutokana na dosari ambazo zilijitokeza wakati wa zoezi ka upigaji kura kwa askari wa nchi hiyo. 

Matangazo ya kibiashara

Misururu mirefu ya askari ilishuhudiwa kwenye maeneo mengi ambayo yalikuwa yakitumika Kama vituo vya kupigia kura kwenye zoezi lililodumu kwa siku mbili kwa askari ambao watakuwa zamu tarehe 31 ya mwezi July mwaka huu ambayo ndio tarehe rasmi ya uchaguzi.

Polisi kadhaa pia walishindwa kupiga kura kutokana na ama kukosa majina yao kwenye daftari, kuchelewa kufika kwa karatasi za kupigia kura na baadhi ya maeneo karatasi hizo kitofika kwa wakati na kusababisha baadhi yao kuondoka.

Akizungumza na wanahabari mjini Harare, katibu mkuu wa chama cha upinzani nchini humo cha Movement For Democratic Change, MDC, Tendai Biti, amesema kasoro zilizojitokeza siku ya Jumapili ni kielelezo tosha kuwa ZEC haiko tayari kufanya uchaguzi mkuu uliopita huru na haki.

Rais Robert Mugabe ambaye amekaa madarakani kwa miaka 33 hivi sasa anaendelea kuwania kiti hicho ambacho iwapo kati yao akaibuka mshindi atamaliza utawala wa Serikali ya muungano iliyoundwa Mara baada ya vurugu za uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wa mwaka 2008/2009.

Waziri mkuu Morgan Tsvangurai na chama chake cha MDC kabla hata ya kutangazwa kwa tarehe ya uchaguzi waliomba uchaguzi huo usogezwe mbele kutokana na tume ya taifa ya uchaguzi nchini hum ZEC kutokuwa tayari kuandaa uchaguzi uliokuwa huru na haki.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa uchaguzi wa mwaka huu nchini Zimbabwe utakuwa wa upinzani licha ya kasoro ambazo zimeshuhudiwa wakati askari wakipiga kura za awali siku ya Jumapili.

Uchaguzi wa Zimbabwe unatazamwa na watu wengi hasa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC ambayo ndio ilisaidia kupatikana kwa suluhu ya kusiasa nchini Zimbabwe mara baada ya kutokea machafuko.