INDIA

Watoto 21 wapoteza maisha nchini India baada ya kula chakula kinachodaiwa kuwa na sumu

Wanafunzi nchini India wakiwa wanapata chakula cha mchana
Wanafunzi nchini India wakiwa wanapata chakula cha mchana Reuters

Zaidi ya watoto ishirini na mmoja wamepoteza maisha nchini India kufuatia kula chakula cha bure walichopewa kwenye shule yao na kuelezwa kuwa huenda kilikuwa na kemikali za sumu.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea kaskazini mashariki mwa nchi ya India kwenye mji wa Bihar ambapo mara baada ya kumaliza vipindi vya mchana watoto hao walipewa chakula ambapo baada ya kula walianza kupoteza nguvu na wengine kupoteza maisha.

waziri wa elimu kwenye mji huyo, P.K. Shahi amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari uchunguzi umeanza kubaini aina ya chakula na sumu ambayo huenda ilikuwa imewekwa kwenye chakula chao.

Watoto hao ishirini wamezikwa asubuhi ya hii leo jirani na eneo la shule huku wengine zaidi ya thelathini wakiwa hospitalini kupatiwa matibabu baada ya kuwahishwa kufika kwenye kituo cha afya.

Wananchi kwenye eneo hilo wameandamana nje ya shule hiyo huku wakiharibu miundombinu yake wakitaka waliohusika na kuwapa chakula watoto hao kuchukuliwa hatua za kisheria.

Uchunguzi wa awali tayari umeanza kufanywa ambapo polisi inadai kuwa huenda chakula hicho kilikuwa na kemikali inayotumiwa kutengeneza mbolea.

Nchi ya India ni moja kati ya mataifa ambayo wananchi wake wa vijijini wananchi kwenye hali ngumu huku wengi wakishindwa kupata mlo kamili.