TALIBAN-MALALA-PAKISTAN

Kundi la Taliban lamwandikia barua Malala kumtaka arejee nyumbani

Malala Yousafzai mwanaharakati msichana aliyepigwa risasi na kunusurika na wapiganaji wa Taliban
Malala Yousafzai mwanaharakati msichana aliyepigwa risasi na kunusurika na wapiganaji wa Taliban REUTERS/Brendan McDermid

Kiongozi wa kundi la Taliban nchini Pakistan, Adnan Rasheed amemwandikia barua mwanaharakati msichana Malala Yousafzai ambaye alipigwa risasi na wafuasi wa kundi hilo mwaka uliopita. 

Matangazo ya kibiashara

Rasheed kwenye barua yake kwenda kwa Malala ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kuongeza kuwa angeweza kwa wakati huo angemshauri Malala kabla ya wapiganaji wao kumshambulia kwa risasi.

Kwenye barua hiyo ambayo imeonekana sio ya kawaida, Imeeleza ni kwanin wapiganaji wake walitekeleza shambulio la risasi dhidi ya Malala, na kudai kuwa hawapingi watoto kupata elimu lakini wanapinga kampeni inayofanywa na Malala kuhusu kundi la Taliban.

Rasheed ameomba Radha kutokana na shambulio hilo lakini akasema hajutii kupigia risasi kwa Malala kwakuwa anapinga na kuendesha harakati za kupinga mfumo wa utawala wa Shari za kiislamu.

Kiongozi huyo hata hivyo hakuomba radhi kwaniaba ya kundi zima lakini akasema kuwa anaeweza kuhukumu iwapo tukio lile lilikuwa halali au la ni Mwenyezi Mungu peke yake.

Barua hiyo inaandikwa ikiwa zimepita siku chache toka Malala Yousafzai ahutubie mkutano maalumu wa Umoja wa Mataifa UN wakati pia akisherehekea siku yake ya kumaliza juma moja lililopita.

Kundi la Taliban limemtaka Malala arejee nchini mwake lakini aachane na kampeni za kupiga vita kundi hilo pamoja na kukubali kujiunga kwenye madrasa ya shule ya kiislamu na wenzake.