MISRI-EU

Umoja wa Ulaya waitaka Serikali ya mpito nchini Misri kumuachia Mohamed Morsi

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton  akiwa na rais wa mpito wa Misri, Adly Mansour walipokutana jana mjini Cairo
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton akiwa na rais wa mpito wa Misri, Adly Mansour walipokutana jana mjini Cairo REUTERS/Egyptian Presidency/Handout via Reuters

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton amesema kuwa amesikitishwa kutokana na kushindwa kukutana ana kwa ana na rais aliyepinduliwa madarakani, Mohamed Morsi. 

Matangazo ya kibiashara

Ashton ambaye alikuwa kwenye ziara ya kikazi nchini Cairo, amesema kusikitishwa na kuzorota kwa hali ya kisiasa nchini Misri, na kwamba hakikisho la usalama kwa raia linahitajika toka kwa Serikali ya mpito.

Kiongozi huyo akatoa wito kwa Serikali ya mpito inayoongozwa na waziri mkuu Hazem Beblawi kumuachia huru Morsi na wafuasi wengine wa chama chake kwa lengo la kutuliza maandamano yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Ashton amesema kuwa anaamini kiongozi huyo inabidi aachiwe lakini amehakikishiwa kuwa kiongozi huyo yuko salama ambapo yuko kizuizini toka alipokamatwa July 3 mwaka huu baada ya jeshi kuchukua nchi.

Mkuu huyo wa sera za mambo ya nje wa Ulaya amefanya mazungumzo na kiongozi wa juu wa chama cha Muslim Brotherhood, Amr Darrag na kumtaka akubali kushirikiana na Serikali iliyotangazwa Juma hili.

Kabla ya kuondoka nchini humo, Ashton amesema Umoja wa Ulaya unaomkakati wa kuhakikisha machafuko yanamalizika nchini Misri.

Waziri wa fedha wa Misri, Ahmed Galal amesema licha ya machafuko yanayoendelea, shirika la fedha duniani IMF limekubali kuipatia mkopo nchini hiyo wakati huu ikifanya jitihada za kirejesha uchumi wake kwenye hali ya kawaida.

Katika hatua nyingine, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry amekiri kuwa kwasasa huwezi kibashiri hali ya kisiasa nchini humo lakini akasema kuna hata ya nchi hiyo kuwa salama na pande zote mbili kukubali kuketi meza moja kumaliza tofauti zao.

Wakati huo huo, wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood wameendelea na maandamano yao nasasa wameizingira ofisi ya waziri mkuu wakishinikiza kuachiwa kwa kiongozi wao.