UGIRIKI

Wabunge nchini Ugiriki waidhinisha muswada wa sheria mpya ya kubana matumizi

Wafanyakazi nchini Ugiriki wakiandamana nje ya ukumbi wa bunge
Wafanyakazi nchini Ugiriki wakiandamana nje ya ukumbi wa bunge Reuters

Bunge nchini Ugiriki kwa kauli moja limepitisha mswada uliowasilishwa na Serikali kuhusu mpango wake mpya wa ubanaji matumizi ambao utashuhudia maelfunya wafanyakazi nchini humo wakipoteza ajira zao. 

Matangazo ya kibiashara

Wabunge 153 walisema ndio huku wabunge 140 wakikataa kupitisha mswada huo ambao wakati majadiliano yakiendelea, maelfu ya raia walikuwa wamekusanyika nje wakipinga kuidhinishwa kwa mswada huo.

Kusitishwa kwa muswada huo kuwa sheria sasa kutaiwezesha nchi ya Ugiriki kuweza kupatiwa mkopo mwingine unaofikia kiasi cha euro bilioni 6.8 kilichoahidiwa na EU pamoja na IMF Kama sharti la nchi hiyo kupatiwa mkopo.

Muswada huo unawataka wafanyakazi wa umma hasa askari walioajiriwa kwa mkataba kutafuta kazi nyingine wasubiri wasubiri mwisho wa mwezi kuona rungu la Serikali likipita kuwafuta kazi.

Nchi ya Ugiriki imejikuta kwenye maandamano ya mara kwa mara yanayofanywa na wafanyakazi nchini hum ambao wanapinga hatua zaidi ya ubanaji matumizi ambao unasababisha mamia ya vijana kupoteza ajira zao.