MALI

Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye vurugu za mjini Kidal

Vijana wenye asili ya watu weusi kwenye mji wa Kidal wakiwa na bango linalosomeka "Asante kwa ukombozi"
Vijana wenye asili ya watu weusi kwenye mji wa Kidal wakiwa na bango linalosomeka "Asante kwa ukombozi" Reuters

Mtu mmoja ameripotiwa kupoteza maisha na wengine kadhaa wajeruhiwa kufuatia mapigano yaliyozuka kati ya raia wa Mali wenye asili ya watu weusi kwenye mji wa Kidal, na watu wa jamii ya Tuareg. 

Matangazo ya kibiashara

Vurugu hizo zinazuka wakati zikiwa zimebaki siku tisa kabla ya wananchi wa Mali hawajashiriki uchaguzi mkuu huku hali ya usalama kwenye mji wa Kidal ikisalia kuwa tete.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa vikosi vya UN vya kulinda amani kwenye mji wa Kidal, amenukuliwa akisema kuwa vurugu hizo zilizuka baada ya kusambazwa kwa uvumi kuwa Serikali imepeleka wanajeshi zaidi kwenye mji huo.

Mji wa Kidal ndio mji pekee kaskazini mwa Mali ambao wafuasi wa Tuareg wanatishia kuvuruga zoezi la uchaguzi licha ya kutia saini makubaliano ya amani na Serikali.

Miji mingi kaskazini mwa nchi hiyo ilikuwa inakaliwa na makundi ya waislamu wenye msimamo lakini maeneo mengi hali ya usalama imerejea isipokuwa mji wa Kidal ambao vurugu zimeendelea kushuhudiwa.

Watu walioishuhudia tukio hilo wamesema kuwa milio ya risasi ilisikika kati ya wapiganaji wanaodaiwa kuwa ni wa kundi la MNLA na waafrika weusi wanaoishi kwenye wa Kidal.

Ni majuma kadhaa tu yamepita toka watu wa jamii ya watu weusi kwenye mji wa Kidal walalmike kuwa wanatengwa na jamii ya watu wa Tuareg huku kukiripotiwa vurugu baina ya koo hizo mbili.