IVORY COAST-ICC

Mwendesha mashtaka wa ICC akutana na waziri wa sheria wa Cote d'Ivoire kuzungumzia kesi dhidi ya Gbagbo

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya ICC, Fatou Bensouda ambaye yuko nchini Cote d'Ivoire kukusanya ushahidi zaidi dhidi ya Gbagbo
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya ICC, Fatou Bensouda ambaye yuko nchini Cote d'Ivoire kukusanya ushahidi zaidi dhidi ya Gbagbo REUTERS/Thomas Mukoya

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC , Fatou Bensouda yuko nchini Cote d'Ivoire ambapo anakutana na waziri wa sheria wa nchi hiyo kujadili kesi dhidi ya rais wa zamani wa taifa hilo, Laurent Gbagbo. 

Matangazo ya kibiashara

Bensouda anakutana kwa mazungumzo na waziri wa sheria wa nchi hiyo, Gnenema Coulibaly ambapo pamoja na mambo mengine waajadili namna ya kukusanya ushahidi zaidi dhidi ya Gbagbo anashikiliwa kwenye mahakama hiyo.

Ziara ya mwendesha mashtaka nchini Cote d'Ivoire inakuja kufuatia majaji wa mahakama ya ICC wanaosikiliza kesi dhidi ya Gbagbo kumuagiza kwenda nchini humo kukusanya ushahidi zaidi kabla ya kuamua iwapo ana mashtaka ya kujibu au la.

Hatua hiyo imekuja baada ya majaji wanaosikiliza kesi dhidi ya Gbagbo kutoridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na mwendesha mashtaka na kuiagiza ofisi yake kukusanya ushahidi zaidi kabla hawajaamua iwapo Gbagbo ana kesi ya kujibu au la.

Uamuzi huo ulionekana kama pigo kwa ofisi ya mwendesha mashtaka ambayo awali ilidai inaushahidi wa kutosha kumshtaki Gbagbo kutokana na kuhusika kwake wakati wa vurugu za mara baada ya uchaguzi mwaka 2010/2011 wakati akiwa rais.

Kesi ya dhidi ya Gbagbo ilifunguliwa na aliyekuwa mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo, Luis Moreno Ocampo ambaye amemaliza muda wake.

Gbagbo anakabiliwa na makosa ya uhalifu dhidi ya binadamau, kuamrisha mauaji pamoja na vitendo vya ubakaji vilivyofanywa na wanajeshi wake wakati akiwa rais.

Mawakili wa Gbagbo wanasema kesi hiyo inachochewa kisiasa na kwamba ofisi ya mwendesha mashtaka haina ushahidi wa kutosha dhidi ya mteja wao.