UN-DRC-M23

UN: Jeshi la Serikali ya DRC linafanya kazi nzuri mjini Goma kuwadhibiti M23

Wanajeshi wa jeshi la DRC wakijiandaa kuingia kwenye uwanja wa mapambano
Wanajeshi wa jeshi la DRC wakijiandaa kuingia kwenye uwanja wa mapambano Reuters

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, kati ya wanajeshi wa Serikali na waasi wa kundi la M23 ambao wanataka kuushika mji wa Goma.  

Matangazo ya kibiashara

Hapo jana jeshi la DRC lilitoa taarifa kueleza mafanikio makubwa waliyoyapata kwenye vita dhidi ya kundi la M23 na kwamba kwa sehemu kubwa wameweza kuwarejesha nyuma wapiganaji wa M23.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon amelitaka jeshi la FRDC kuheshimu haki za binadamu na kutodhalilisha maiti za wapiganaji wa M23 waliouawa wala kuwanyanyasa mateka ambao inawashikilia.

Katika hatua nyingine, Umoja wa Mataifa UN umesema jeshi maalumu la Umoja huo lililoko masharki mwa DRc liko tayari kukabiliana na makundi ya waasi siku chache baada ya waandamanaji kulituhumu jeshi hilo kushindwa kazi.

Msemaji wa UN, Martin Nesirky amesema kuwa jeshi la MONUSCO halijashirikiana na jeshi la DRC katika kukabiliana na makundi ya waasi kwakuwa wao wanamamlaka maalumu ya kufanya hivyo.

Msemaji huyo akaongeza kuwa kikosi maalumu cha Umoja huo kinachoundwa na wanajeshi wa Tanzania, Malawi na Afrika Kusini kiko tayari kukabiliana na waasi hao na kwamba wanasubiri amri maalumu toka kwenye baraza la usalama la Umoja huo.

Hata hivyo amesema kuwa jeshi la UN litaingilia kati mapigano hayo iwapo itaoenekana usalama wa wananchi wa Goma uko hatarini lakini kwa sasa jeshi la FRDC linafanya kazi nzuri kuwadhibiti wapiganaji hao.

Waandamanaji kwenye mji wa Goma wanavituhumu vikosi hivyo kwa kushindwa kutoa msaada wa kutosha kwa wanajeshi wa Serikali ili kuwawezesha kukabliana na waasi wa M23.