Habari RFI-Ki

Baraza la Mawaziri nchini Sudan Kusini lavunjiliwa mbali huku Makamu wa Rais naye akifukuzwa

Sauti 09:53
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye amelivunjilia mbali Baraza la Mawaziri na kumfuta kazi Makamu wa Rais Riek Machar
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye amelivunjilia mbali Baraza la Mawaziri na kumfuta kazi Makamu wa Rais Riek Machar

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amelivunja Baraza lake la Mawaziri na kisha kumfuta kazi Makamu wa Rais Riek Machar anayetajwa alishatangaza nia ya kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri na kufukuzwa kwa Makamu wa Rais Machar kumezua hali ya wasiwasi huku Jeshi likiimarisha doria na kuwataka wananchi kuwa watulivu!!