Wananchi wa Mali wanatarajiwa kupiga kura kumchagua rais wa Taifa hilo mwishoni mwa juma hili

Sauti 14:21
Masanduku ya kupigia kura ambayo yanatarajiwa kutumika kwenye uchaguzi mkuu wa rais mwishoni mwa juma
Masanduku ya kupigia kura ambayo yanatarajiwa kutumika kwenye uchaguzi mkuu wa rais mwishoni mwa juma AFP/Georges Gobet

Wananchi wa Mali wanatarajiwa kushiriki kwenye Uchaguzi wa Urais utakaofanyika mwishoni mwa juma hili kipindi hiki wakiendelea kukabiliwa na changamoto zikiwemo za kiusalama huku wagombea wakiendelea na kampeni za mwishoni kunadi sera zao. Hofu kubwa imeendelea kusalia iwapo wananchi wa Mji wa Kidal watapigakura au la!! Makala ya Mjadala wa Wiki juma hili yanaangalia hilo pamoja na wachambuzi akiwemo Abdulkarim Atiki na Francis Onditi!!