Zolani Mahola mwamuziki wa miondoko ya kiafrika anayefanya vizuri nchini Afrika Kusini
Imechapishwa: Imehaririwa:
Sauti 10:16
Makala ya Muziki Ijumaa juma hili inajitupa ugani kumuangalia Mwanamuziki wa Miondoko ya Kiafrika kutoka nchini Afrika Kusini katika Mji wa Port Elizabeth anayetambulika kwa jina la Zolani Mahola. Zolani ni Mwimbaji katika Bendi iitwayo Fleshly Ground, Bendi ya Kiafrika iliyoundwa jijini Cape Town mwaka 2002 wanamuziki wanaounda Bendi hiyo ambayo Zolani ni mwimbaji Kiongozi wanatoka nchini Afrika kusini, Msumbiji na Zimbabwe.