Mataifa jirani na DR Congo yatakiwa kusitisha ufadhili kwa Kundi la M23 huku wanajeshi saba wa Tanzania waliouawa Darfur wakizikwa

Sauti 20:10
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ambao wamezitaka nchi jirani na DR Congo kuacha kulifadhili Kundi la Waasi la M23
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ambao wamezitaka nchi jirani na DR Congo kuacha kulifadhili Kundi la Waasi la M23

Marekani na Umoja wa Mataifa UN wamenyoosha kidole chao na kuzielekea nchi jirani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuacha mara moja kuwafadhili Waasi wa M23 ambao wanapambana na Jeshi la Serikali la FARDC katika eneo la Mashariki, Serikali ya Tanzania yautaka Umoja wa Mataifa UN kuhakikisha wanatoa nguvu zaidi kwa wanajeshi wa kulinda amani waliopo katika Jimbo lenye machafuko la Darfur ili waweze kujilinda pale ambapo wanashambuliwa na Umoja wa Mataifa UN watoa takwimu zinazoonesha watu zaidi ya 100,000 wamepoteza maisha katika kipindi cha miezi 28 nchini Syria kunakoshuhudiwa umwagaji mkubwa wa damu!!