ZIMBABWE

Rais Mugabe ahaidi kutekeleza aliyoahidi, hofu ya mgawanyiko ndani ya chama cha upinzani MDC-T yatanda

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe Reuters

Rais wa Zimbabwe Comrade. Robert Gabriel Mugabe amesema tahakikisha anatekeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni za kuwania kiti hicho na kwamba wananchi watarajie mambo makubwa.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwa mara ya kwanza Jumatano hii toka atangazwe kuwa mshindi wa kiti hicho, rais Mugabe amesema kuwa ushindi wake ni pigo kwa mataifa ya magharibi na maadui wa nchi yake.

Rais Mugabe ameongeza kuwa anafahamu kuwa mataifa mengi ya magharibi walitarajia kuona anashindwa kwenye uchaguzi huu lakini wananchi wa Zimbabwe wameongea kupitia njia ya debe kwa kumrejesha tena madarakani kwakuwa wanaumani nae.

Akimzungumzia mpinzani wake waziri mkuu Morgan Tsvangirai, rais Mugabe anasema kuwa kiongozi huyo sio adui yake namba moja kwahivyo hamuumizi kichwa kama mataifa ya magharibi ambayo yameendelea kukashifu ushindi wake.

Rais Mugabe anaituhumu nchi ya Uingereza kwa kuendelea kumfadhili mpinzani wake Moragn Tsvangirai ili ashinde kwenye uchaguzi huo zoezi ambalo rais Mugabe anasema limeshindikana.

Katika hatua nyingine wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa waziri mkuu Morgan Tsvangirai huenda akakabiliwa na mgawanyiko mkubwa ndani ya chama chake kwakuwa tayari kuna baadhi ya wabunge wameonesha nia ya kushirikiana na Serikali kinyume na matakwa ya rais wao ambae ameahidi kutoshirikiana na Serikali.

`rais Robert Mugabe alishinda

Zimbabwe's electoral commission declared Mugabe winner with 61 percent of the vote, while three-time presidential hopeful Tsvangirai garnered 34 percent.