SYRIA

Serikali ya Syria yakanusha msafara wa rais Assad kushambuliwa leo asubuhi

Rais Bashar al-Assad akisali kwenye moja ya msikiti ambao huwa anautumia hivi karibuni
Rais Bashar al-Assad akisali kwenye moja ya msikiti ambao huwa anautumia hivi karibuni Reuters

Kumeripotiwa mashambulizi kwenye viunga vya jiji la Damascus na makazi ya rais Bashar al-Assad, mashambulizi ambayo yalilenga pia msafara wake. 

Matangazo ya kibiashara

Waangalizi wa kutetea haki za binadamu kwenye mji wa Malki ambako yako makazi ya rais Assad pamoja na makazi yake, wameeleza kusikia milipuko mikubwa kwenye maeneo jirani na makazi ya rais.

Mbali na makazi ya rais Assad kulengwa kwenye mashambulizi ya leo asubuhi, pia mashambulizi mengine yalilenga msafara wake ambapo mapaka sasa hakuna taarifa iwapo kuna mtu yeyote amejeruhiwa kwenye matukio hayo.

Hata hivyo licha ya taarifa kuwa msafara wa rais Assada ulishambuliwa leo asubuhi, waziri wa habari nchini humo amekanusha taarifa hizo na kwamba hakuna shambulio lolote lililotekelezwa dhidi ya makazi ya rais.

Serikali imeonesha mkanda wa video ukimuonesha rais Assad akiuwa na maofisa wengine wa Serikali wakifanya sala ya Eid al-Fitr kwenye msikiti wa Ummayad ambao awali uliriptiwa kushambuliwa.

Kundi la kiislamu la Liwa al-Islam limedhibitisha kuhusika na mashambulizi ya jirani na makazi ya rais na kwamba walilengamsafara wa rais uliokuwa ukielekea kwenye msikiti huo.

Mashambulizi haya yanakuja wakati hapo jana kukiripotiwa kuuawa kwa wapiganaji zaidi ya thelathini wa waasi kufuatia shambulizi la kushtukiza lililofanywa na wanajeshi wa Serikali.