NIGERIA

Askari wa Nigeria aliyenaswa kwenye picha ya video akipokea rushwa afukuzwa kazi

Askari nchini Nigeria wamekuwa wakituhumiwa kwa kukithiri kupokea rushwa toka kwa madereva
Askari nchini Nigeria wamekuwa wakituhumiwa kwa kukithiri kupokea rushwa toka kwa madereva Reuters

Afisa mmoja wa polisi nchini Nigeria anaedaiwa kupokea rushwa ya dola 115 na video yake kuonekana kwenye mtandao wa youtube amefutwa kazi na leo amepandishwa kizimbani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Matangazo ya kibiashara

Kukamatwa na kufutwa kazi kwa afisa huyu wa polisi imeonekana kama kitendo cha kwanza kuwahi kufanyika hadhari kwa vyombo vya usalama kumkamata afisa mwenzao na kumfikisha mahakamani kwa makosa ya rushwa.

Picha za video ambazo zilisambazwa kwenye mtandao zilimuonesha afisa huyo akipokea hongo ya dola 155 toka kwa dereva wa daladala na kisha kumwachia kitendo ambacho kilifanya hata mashirika yanayopamabana kupiga vita rushwa kuingilia kati.

Makundi ya wanaharakati nchini humo wanadai kuwa pindi polisi hao wakipokea rushwa toka kwa madereva wa mabasi, kiasi kidogo cha fedha hukipeleka kwa maofisa wao wa juu na yeye kusalia na kiasi kingine tuhuma ambazo hata hivyo jeshi la polisi nchini humo limekanusha.

Msemaji wa jeshi la Polisi nchini Nigeria, Frank Mba amedhibitisha kufutwa kazi kwa askari huyo na kuongeza kuwa tayari hii leo amepandishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.

Jeshi la Polisi nchini Nigeria ni moja kati ya taasisi ambazo zinatuhumiwa nchini humo kwa kukithiri kwa vitendo vya rushwa.