DRC-RWANDA

Rwanda inafikiria ombi la kurejeshwa nchini DRC kwa wapiganaji 4 wa kundi la M23

Kiongozi wa kundi la M23 lililojitenga, Jean-Marie Runiga ambaye amekimbilia nchini Rwanda kuomba hifadhi
Kiongozi wa kundi la M23 lililojitenga, Jean-Marie Runiga ambaye amekimbilia nchini Rwanda kuomba hifadhi AFP PHOTO / Junior D.Kannah

Mamlaka nchini Rwanda inalifanyia kazi ombi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kutaka raia wake wanne wa kundi la M23 walioko nchini humo warejeshwe nyumbani, wizara ya mambo ya nje ya Rwanda imesema.  

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wanahabari mjini Kigali, waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda Louise Mushikiwabo amedhibitisha nchi yake kupokea maombi rasmi toka kwa Serikali ya DRC wakiomba watuhumiwa wanne wa kundi la M23 wanaoishi nchini humo warejeshwe nyumbani.

Waziri Mushikiwabo amesema kuwa wao kama Serikali wamepokea ombi hilo na wanalifanyia jkazi kuangalia uwezekano wa kuruhusi wapiganaji hao wa kundi la waasi warejeshwe nchini DRC kwenda kukabiliana na mashtaka yao.

July 25 mwaka huu Serikali ya Rwanda ilitoa hati nne za kukamatwa kwa viongozi wa kundi la M23 waliokimbilia nchini humo wakitokea nchini DRC ambako kundi lao linapamabana na wanajeshi wa Serikali huku kati yao wakiwa wamelikacha kundi hilo.

Kwenye maombi hayo ya Serikali ya DRC, wanaomba kurejeshwa nyumbani kwa Jean-Marie Runiga aliyekuwa msemaji wa kisiasa wa kundi hilo, Kanali Baudouin Ngaruye ambaye alikuwa jenerali wa M23, wengine ni Eric Badege na kanali Innocent Zimurinda.

Kundi la M23 linaundwa na wanajeshi wa zamani wa kitutsi ambao walijiondoa kwenye jeshi la Serikali mwaka 2009 na kisha kujiunga na tena mwaka 2012 na kulifanya kundi hilo kutekeleza haralati zake kwenye jimbo la Kivu Kaskazini.

Mwezi February mwaka huu baadhi ya viongozi wa kundi hilo walijitenga kwenye makundi mawili kukawa na wale wanaomuunga mkono kamanda Sultan Makenga na wale wanaomuunga mkono Runiga.

Kujitenga kwa kundi hilo kulisababisha zaidi ya wapiganaji 700 wa kundi la Runiga kukimbia nchini DRc na kuingia nchini Rwanda kuomba hifadhi.

Mapigano hayo pia yalipelekea kujisalimisha kwa Jenerali Bosco Ntaganda aliyekimbilia kwenye ubalozi wa Marekani mjini Kigali kabla ya kupelekwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC.