QUETTA-PAKISTAN

Tisa wauawa kwenye shambulio la risasi mjini Quetta, Pakistan, Marekani yawahamisha maofisa wake Lahore

Moja ya mashambulizi yaliyofanywa hivi karibuni kwenye mji wa Quetta nchini Pakistan
Moja ya mashambulizi yaliyofanywa hivi karibuni kwenye mji wa Quetta nchini Pakistan REUTERS/Naseer Ahmed

Mtu mmoja mwenye silaha amewaua watu tisa kwa kuwafyatulia risasi wakati wakitoka msikitini kuhudhuria sala ya Eid al-Fitr kwenye msikiti wa Quetta kusini mwa nchi ya Pakistan, Polisi wamedhibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili kwenye mji wa Quetta lililenga waumini wa madhehebu ya Kisuni ambao walikuwa wakitoka kwenye sala ya sikukuu ya Eid al-Fitr na ndipo mtu mwenye silaha akaanza kuwashambulia.

Shambulio la hivi leo linakuja ikiwa imepita siku moja tu toka kushuhudia shambulia baya zaidi kwenye mji huo ambapo watu 38 waliuawa kwenye shambulio la bomu la kujitoa muhanga kwenye mji huo.

Shambulio hili linafanya mpaka kufikia sasa watu 120 kupoteza maisha toka mwaka huu uanze kwenye mashambulizi zaidi ya kumi na moja yaliyotekelezwa na makundi ya kigaidi nchini humo.

Polisi wanasema kuwa watu wanne waliokuwa na silaha walisimama mbele ya msikiti ambao ulikuwa unatumika kwa sala ya Eid na kuanza kuwafyatulia risasi waumini waliokuwa wakitoka mara baada ya kumaliza sala yao.

Polisi wameongeza kuwa huenda shambulio hilo lilimlenga waziri wa zamani wa jimbo hilo, Ali Madad Jatak ambaye alikuwa akisali kwenye msikiti huo wakati shambulio hilo likitekelezwa.

Tayari Serikali ya Marekani imewataka raia wake wanaosafiri kwenda nchini Pakistan kutofanya hivyo pamoja na kutangaza kuufunga ubalozi wake wa mjini Lahore nchinbi Pakistan kufuatia vitisho vya mashambulizi ya mabomu toka kwa wanamgambo wa Taliban.