SYRIA-MAPIGANI

Jeshi la Syria limekanusha taarifa za kutumia bomu za sumu katika shambulio moja huko Damascus lililo sababisha vifo vya watu 1300

wataalamu wanachunguza miili ya watu wanadaiwa kuuawa kwa bomu za sumu Agosti 21 katika viunga vya jiji la Damascus.
wataalamu wanachunguza miili ya watu wanadaiwa kuuawa kwa bomu za sumu Agosti 21 katika viunga vya jiji la Damascus. REUTERS/Bassam Khabieh

Jeshi la Syria limekanusha kutumia bomu za sumu katika mashambulizi yake ya kwenye viunga vya mji mkuu Damascus, kama linavyo tuhumiwa na upinzani ambao ulitowa taarifa ya mauaji ya ma mia ya watu kufuatia bomu hizi za sumu. Katika taarifa iliotolewa na jeshi na kusomwa na afisaa moja wa jeshi nchini Syria, imesema, shutma kwa jeshi la Syria za matumizi ya bomu za sumu dhidi ya waasi hazina msingi wowote

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo imesema, vikosi vya upinzani vimepata pigo kubwa sana katika uwanja wa mapambano, hivo unataka kuficha ukweli kuhusu hali tete iliopo wakati huu upande wao, na kuzua taarifa zisizokuwa na ushahidi wowote na kupeperushwa na vyombo vya habari vinavyowaunga mkono.

Taarifa hiyo imesema jeshi la serikali litaendelea na jukumu lake la kitaifa la kuwalinda raia dhidi ya aduwi anaye patikana katika ardhi ya Syria na kurejesha maeneo yote yaliokaliwa na maaduwi hao.

Upinzani ncini Syria umaituhumu serikali ya Dascus kwa kutumia bomu zenye sumu siku ya Jumatano katika viunga vya jiji la Damacus na kusababisha ma mia kupoteza maisha.

Upinzani huo umewataka wataalamu wa Umoja wa Mataifs ambao wapo nchini Syria kuelekea katika eneo la tuki kushuhudia.

Wakati huo huo mkuu wa sera za mambo ya nje wa serikali ya Saudia Arabia mwanamfalme Saoud al Faycal ameliomba baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kwa dharura kujadili kuhusu mauaji yasliotkea leo jijini Damascus.

Al Faycal amesema baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatakiwa kufanya kikao hara iwekanavyo na kuchukuwa maamuzi ambayo yatapelekea kukomeshwa kwa umwagaji wa damu na kuwataka viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaokutana jijini Brusels kuzungumzia hali inayoendelea nchini Misri, kulipa kipao mbele swala hilo la mashambulizi nchini Syria.

Upinzani Syria umethibitisha kuwa vikosi vya serikali ya rais bashar al Assad vimetumia bomu za sumu katika amshambulzi yao leo mjini Damascus yaliosabaisha vifo vya watu 1.300, taarifa inayoendelea kukanushwa na serikali.