MISRI-MAHAKAMA

Mahakama nchini Misri kusikiliza kesi ya uchochezi dhidi ya makam wa rais aliejiuluzu, huku ikipitia upya ombi la kuachiwa huru kwa rais Hosni Mubarak

Mohamed Elbaradai, makam wa rais wa serikali ya mpito aliye jiuzulu
Mohamed Elbaradai, makam wa rais wa serikali ya mpito aliye jiuzulu

Mahakama kuu nchini Misri inapanga tarehe ya kuanza kusikiliza kesi ya uchochezi na kutishia usalama wa taifa dhidi ya aliyekuwa makamu wa rais wa serikali ya mpito Mohammed Elbaradei aliyetangaza kujiuzulu juma moja lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Mashitaka hayo ya kuisalaiti nchi yamefunguliwa na profesa mmoja ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Helwan cha mjini Cairo akidai kuwa ELBARADEI alikiuka misingi ya uongozi na kuusaliti umma wa nchi hiyo.

Kama atakutwa na hatia ELBARADEI atakabiliwa na faini ya dola 1,430.

Hayo yanakuja huku mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za umoja wa ulaya wakielekeza nguvu zao kusaka njia ya kuisaidia misri iondokane na mgogoro huo.

Katika hatuwa nyingine Mahakama kuu nchini humo imesema inapitia upya maombi yaliyowasilishwa na mawakili wa rais wa zamani wa taifa hilo Hosni Mubarak kutaka kiongozi huyo kuachiwa huru baada ya kufutiwa mashtaka ya rushwa.

Mwishoni mwa juma mahakama hiyo ilimfutia kosa la tatu la matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kubakisha kesi moja ya rushwa, keso ambayo hata hivyo mawakili wake wamekata rufaa huku kukiwa na matumaini makubwa ya kionfozi huyo kuachiwa.

Tayari wasiwasi umeibuka nchini humo kuwa huenda Hosni Mubaraka akaachiwa huru licha ya kesi ya kuamrisha mauaji inayomkabili wakati alipoondolewa madarakani mwaka 2011 kwa maandamano.